[go: up one dir, main page]

Nenda kwa yaliyomo

Lego

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Matofali ya Lego.
Mfano wa Trafalgar Square (London) huko Legoland.

Lego ni kampuni ya Denmark inayotengeneza vichezeo mashuhuri ya "Lego". Kampuni ni mtengezaji mkubwa wa vichezeo duniani.

Matofali ya plastiki

[hariri | hariri chanzo]

Lego ni hasa matofali madogo ya plastiki yanayoweza kuunganishwa kuunda mifano ya kila kitu.

Kiasili kampuni ilitengeneza michemraba ya ubao na tangu mwaka 1949 mtindo huu ulipanuliwa kwa kutumia plastiki.

Baada ya kufaulu, chaguo la vipande vya kuunganishwa liliongezeka kuwa pamoja na mwanaserere ndogo zenye kichwa, mwili wa juu na mwili wa chini pekee, hivyo zinaweza kutenganishwa na kuunganishwa upya, na magurudumu na vipande vingine kwa kuunda gari. Kuna pia mikusanyo ya vipande vya nyongeza vinavyoruhusu kuunda mifano ya miji, anga-nje, jahazi na meli, maboma, masauri, na mengine mengi.

Lego Technic

[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 1977 Lego ilipanuliwa tena kwa vipande vya Lego Technic iliyoongeza injini za umeme, kompresa na pampu za hewa zilizoruhusu kuunda mifano ya trekta au mashine nyingine.

Roboti za Lego

[hariri | hariri chanzo]

Mtindo huu umepanuliwa katika karne ya 21 kwa vipande vya "Lego Mindstorm" vinavyoruhusu kutengeneza roboti. Kiini chake ni tofali lenye chipu ndani yake inayopokea amri kupitia kompyuta ya nyumbani na amri zinatekelezwa kwa kutumia injini ya umeme na vigunduzi mbalimbali vya nuru, sauti na mgusano.

Kampuni ilianzisha pia miradi ya kitalii ya Legoland ambako mifano ya majengo mashuhuri ya dunia yanaonyeshwa ambayo yameundwa kwa matofali ya Lego.

Mifano ya matumizi ya Lego

[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lego kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.