Karachi
Kaburi la Baba wa Taifa Mohammed Ali Jinnah (1876-1948) mjini Karachi (Pakistan) | |
Jimbo | Sindh |
Anwani ya kijiografia | Latitudo: 24°51'3"N - Longitudo: 67°1'5"E |
Kimo | 22 m juu ya UB |
Eneo | 591 km² (mji pekee) 3,527 km² (wilaya ya Karachi) |
Wakazi | 11,969,284 (2006) |
Msongamano wa watu | watu 3,394 kwa km² watu 18,000/km² mjini pekee |
Simu | +92 (nchi), 21 (mji) |
Mahali | |
Karachi (Kiurdu: كراچى) ni mji mkubwa wa Pakistan na mji mkuu wa jimbo la Sindh. Hadi 1959 ilikuwa mji mkuu wa kitaifa. Mji ni kitovu cha kibiashara cha Pakistan.
Karachi iko kando la delta ya mto Indus mwambaoni wa Bahari Arabu. Kuna mabandari mawili na viwanda vingi.
Mohammed Ali Jinnah anayekumbukwa kama baba wa taifa la Pakistan alizaliwa pia kuzikwa mjini.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Eneo la Karachi lilikaliwa na watu tangu muda mrefu na miji mbalimbali ya kihistoria imeaminiwa kuwepo katika eneo lake tangu zamani za Aleksander Mashuhuri aliyepita hapa. Katika karne ya 17 palikuwa na kijiji cha wavuwi kilichoitwa "Kolachi". Kikakua kuwa bandari ya biashara na Bara Arabu. Baada ya kuungwa kwa Sindh katika Uhindi wa Kiingereza mnamo 1843 Waingereza waliona nafasi nzuri ya bandari hiyo wakaanza kupanga na kukuza mji. 1864 mawasiliano ya simu ilianzishwa kati ya Karachi na London. 1878 mji ukaunganishwa na reli za Uhindi. Mwisho wa karne ya 19 idadi ya wakazi ilipita lakhi moja.
Wakati wa utengano wa Uhindi wa Kiingereza nusu ya wakazi walikuwa Wahindu waliopaswa kukimbia Uhindi. Wakimbizi Waislamu kutoka Uhindi walichukua nafasi yao wako sasa takriban nusu ya wakazi wote wa mji.
Baada ya Uhuru wa Pakistan Karachi ilikuwa mji mkuu hadi 1959.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Official Karachi website Archived 25 Machi 2002 at the Wayback Machine.
- Quaid-e-Azam International Airport
- Karachi Port Trust
- Photographs by HistoricKarachi.com Archived 22 Agosti 2008 at the Wayback Machine.
- Photogrphs by Flickr.com