9 Machi
Mandhari
Feb - Machi - Apr | ||||||
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
29 | 30 | 31 | ||||
Kalenda ya Gregori |
Tarehe 9 Machi ni siku ya 68 ya mwaka (ya 69 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 297.
Matukio
[hariri | hariri chanzo]- 1513 - Uchaguzi wa Papa Leo X
Waliozaliwa
[hariri | hariri chanzo]- 1285 - Go-Nijo, mfalme mkuu wa Japani (1301-1308)
- 1451 - Amerigo Vespucci, mpelelezi kutoka Hispania
- 1568 - Mtakatifu Aloysius Gonzaga, mtawa kutoka Italia
- 1923 - Walter Kohn, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Kemia mwaka wa 1998
- 1930 - Ornette Coleman, mwanamuziki kutoka Marekani
- 1934 - Yuri Gagarin, rubani Mrusi na mtu wa kwanza aliyefika katika anga-nje
- 1959 - Takaaki Kajita, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 2015
Waliofariki
[hariri | hariri chanzo]- 1440 - Mtakatifu Fransiska wa Roma, mtawa kutoka Italia
- 1463 - Mtakatifu Katerina wa Bologna, bikira Mfransisko kutoka Italia
- 1857 - Mtakatifu Dominiko Savio, kijana wa Italia
- 1888 - Kaisari Wilhelm I, mfalme wa Prussia na Kaisari wa Ujerumani
- 1964 - Paul von Lettow-Vorbeck, mwanajeshi wa Dola la Ujerumani, hasa nchini Tanzania
- 1974 - Earl Sutherland, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1971
- 1981 - Max Delbruck, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1969
- 1983 - Ulf von Euler, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 1970
- 1988 - Kurt Georg Kiesinger, Chansela wa Ujerumani (1966-1969)
- 1997 - The Notorious B.I.G., mwanamuziki kutoka Marekani
Sikukuu
[hariri | hariri chanzo]Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu za watakatifu Fransiska wa Roma, Askari wafiadini wa Kapadokia, Pasiano, Vitale wa Castronovo, Bruno wa Querfurt, Katerina wa Bologna, Dominiko Savio, Petro Ch'oe Hyong na Yohane Mbatizaji Chon Chang-un n.k.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- BBC: On This Day
- On This Day in Canada Archived 2012-12-10 at Archive.today
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu 9 Machi kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |