Jihadi
Jihadi ni neno lenye asili ya Kiarabu (جهاد jihād) na lenye maana ya kujitahidi kwa ajili ya Allah katika dini ya Uislamu.
Mtu anayehusika katika jihadi huitwa "mujahid". Jihadi ni wajibu wa kidini kwa Waislamu.
Jihadi katika Qurani
haririKatika Qurani neno jihadi linapatikana mara 41, mara nyingi katika usemi "jihadi kwenye njia ya Mungu (الجهاد في سبيل الله al-jihad fi sabil Allah)".[1][2][3]. Katika Qurani "jihadi" huwa hasa na maana ya kijeshi[4] lakini si wazi kama maana hiyo ilikuwa mapigano dhidi ya wenye imani tofauti kwa jumla au vita vya kujihami tu.
Jihadi katika mafundisho ya wataalamu wa shari'a
haririKatika mafundisho ya wataalamu Waislamu wa karne za kwanza baada ya Muhammad jihadi ilikuwa na shabaha ya kupanua eneo chini ya utawala wa Uislamu na utetezi wake, hadi Uislamu ugeuke dini rasmi.[5]
Hii haikuwa na shabaha ya kuwalazimisha wote wasiokuwa Waislamu kupokea dini hiyo. Katika mafundisho ya wataalamu wa kale, wale walioitwa "Wapagani" walipaswa kushambuliwa hadi wakubali Uislamu au wauawe. Lakini watu wa "ahl al-kitab" (wenye misahafu) yaani Wakristo, Wayahudi na Wasabayi walipewa nafasi ya kukubali kipaumbele cha Waislamu na kuishi chini ya utawala wa Waislamu katika hali ya dhimma.
Katika mwendo wa upanuzi wa utawala wa Kiislamu nafasi ya dhimma iliongezwa pia kwa dini nyingine kama Uzoroastro na Uhindu ingawa hao wana miungu mingi sana.
Mwishoni karibu kila jumuiya ya kidini ilipewa nafasi ya kukubali hali ya dhimma. [6]
Jihadi kati ya Waislamu wa leo
haririLeo hii jihadi ina maana tatu kati ya Waislamu, hasa
- kutetea imani ya Kiislamu pamoja na kulinda umma ya Waislamu, pia kutetea Waislamu wanaoshambuliwa
- kushindana na udhaifu wa nafsi na kujitahidi kuwa mtu mwema
- jitihada za kuboresha umma ya Waislamu.[7]
Waislamu kadhaa wanaitumia pia kwa maana ya kueneza Uislamu kwa njia ya silaha na matishio. Hapo kuna hata makundi kama Al Qaida na Boko Haram wanaotumia mbinu za ugaidi kwa jihadi jinsi wanavyoielewa. Ingawa idadi yao si kubwa kati ya Waislamu kwa jumla, watu wengi nje ya Uislamu wanaelewa neno hasa kwa maana inayotangazwa na hao.
Tanbihi
hariri- ↑ Morgan, Diane (2010). Essential Islam: a comprehensive guide to belief and practice. ABC-CLIO. uk. 87. ISBN 0313360251. Iliwekwa mnamo 5 Januari 2011.
{{cite book}}
: Cite has empty unknown parameter:|coauthors=
(help); More than one of|pages=
na|page=
specified (help) - ↑ Wendy Doniger, ed. (1999). Merriam-Webster's Encyclopedia of World Religions. Merriam-Webster. ISBN 087-7790442., Jihad, p.571
- ↑ Josef W. Meri, ed. (2005). Medieval Islamic Civilization: An Encyclopedia. Routledge. ISBN 041-5966906., Jihad, p.419
- ↑ Rudolph Peters: Jihad in Classical and Modern Islam. Markus Wiener Publishing Inc., 2005. S. 2. Vgl. Fred M. Donner: The Sources of Islamic Conceptions of War. In: John Kelsay und James Turner Johnson (ed.): Just War and Jihad: Historical and Theoretical Perspectives on War and Peace in Western and Islamic Traditions. Greenwood Press, 1991. S. 47
- ↑ Linganisha: The Encyclopaedia of Islam. New Edition. Brill, Leiden. Bd. 2, S. 538 („Djihad“): „In law, according to general doctrine and in historical tradition, the djihād consists of military action with the object of the expansion of Islam and, if need be, of its defence.“
- ↑ Robert Hoyland (Hrsg.): Muslims and Others in Early Islamic Society. Ashgate, 2004. p. xiv.
- ↑ "Jihad". BBC. 2009-08-03.
Kujisomea
hariri- DeLong-Bas, Natana J. (2004). Wahhabi Islam: From Revival and Reform to Global Jihad (tol. la First). New York: Oxford University Press. ISBN 978-0195169911.
- ibn Abd al-Wahhab, Muhammad (1398h). Kitab al-Tawhid, volume I of Mu'allafat al-Shaykh al-Imam Muhammad Ibn Abd al-Wahahb (tol. la First). Riyad: Jamiat al-Imam MUhammad bin Saudi al-Islamiyah.
- Kadri, Sadakat (2012). Heaven on Earth: A Journey Through Shari'a Law from the Deserts of Ancient Arabia. London: Macmillan Publishers. ku. 150–151, 157, 172–175. ISBN 978-0099523277.
- Qutb, Sayyid (1988). Milestones (PDF). Karachi: International Islamic Publishers. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2021-01-19.
{{cite book}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - H.R.H. Prince, Ghazi Muhammad; Ibrahim, Kalin; Mohammad Hashim, Kamali (2013). War and Peace in Islam: The Uses and Abuses of Jihad (PDF). The Islamic Texts Society Cambridge. ISBN 978-1903682838. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-07-09. Iliwekwa mnamo 2017-06-12.
{{cite book}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - Gerges, Fawaz A. (2009). The far enemy: why Jihad went global (tol. la reprint 2010). New York: Cambridge University Press. ISBN 978-0521519359.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |